CCM Wajibu Mapigo Zanzibar.......Wasema Uchaguzi Lazima Urudiwe
Mpekuzi blog
Muda
mfupi baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif
Sharif Hamad kutangaza kasoro na athari za kurudia Uchaguzi uliofutwa
kinyume cha sheria na Jecha Salim Jecha, viongozi wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) wametangaza kuwa uchaguzi huo lazima urudiwe.
Wakizungumza
jana na vijana wa chama cha Mapinduzi katika viwanja vya Maisara
waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya matembezi ya kuunga mkono Mapinduzi
ya Zanzibar,viongozi wa juu wa chama hicho walisisitiza kuwa uchaguzi
wa Zanzibar upo pale pale na utarudiwa kadiri tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar (ZEC) itakavyotangaza.
Wa
kwanza kutoa msimamo huo alikuwa ni Makamu wa pili wa Rais, Balozi Seif
Ali Iddi, aliyesema kuwa uchaguzi huo utarudiwa hata ikiwezekana vyama
vyote vikijitoa CCM kitashiriki peke yake
“Uchaguzi
wa marudio upo pale pale, tunajua uchaguzi ulifutwa kihalali,
mjitayarishe kwa uchaguzi wa marudio. CUF wamesema watatumia nguvu ya
umma, tunawakaribisha na wataona matokeo yake” alisema Balozi Iddi.
Katika
mkutano huo uliokuwa unarushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni
cha ZBC, Dk Alli Mohamed Shein alipongeza msimamo wa Balozi Iddi, na
kusema atabaki kuwa rais hadi uchaguzi utakaporudiwa.
Dk
Shein alisema yupo madarakani kwa kushauriwa na Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar kwamba hajavunja katiba na kama itatokea mahakama ikatoa
ufafanuzi kuwa anakosea kuwepo hapo kikatiba basi ataondoka madarakani
“Mahakama
ikisema nakosea nitaondoka, Rais yupo Baraza la Mapinduzi lipo na
Mawaziri wapo, nitaita waandishi wa habari Ikulu na mimi nimjibu Maalim
Seif kwani kuna mengi amenisingizia” alisema.
No comments:
Post a Comment