Wednesday, January 13, 2016


MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP) ameamua kukata rufaa Mahakama Kuu dhidi ya kesi ya uchochezi inayomkabili mwanaharakati wa Kiislamu Shehe Ponda Issa Ponda.
Mwanasheria Mwandamizi katika ofisi ya DPP, Bernard Kongola amesema kuwa Serikali inapinga kuachiwa kwa Shehe Ponda ambaye alishitakiwa kwa makosa ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.
“Tayari tumeomba tupatiwe nakala ya hukumu pamoja na nyaraka za mwenendo wa shauri hilo ili upande wa mashitaka tuweze kuandaa rufaa yetu Mahakama Kuu,” alisema.
Kwa mujibu wa mwanasheria huyo, tangu waombe kupatiwa nakala ya hukumu hiyo katika mahakama hiyo ya hakimu mkazi, hakimu ambaye alikuwa anasikiliza kesi hiyo bado hajawapatia upande wa mashitaka hukumu ambayo imechapwa.
“Hatujui kuna tatizo gani, maana tunapoomba kupatiwa nakala ya hukumu, hakimu amekuwa anatuambia kwamba bado hawajamaliza kuichapa, kwa kweli hii inashangaza,” alisema.
Novemba 30 mwaka uliopita, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Morogoro, Mary Moyo alimwachia huru Shehe Ponda kwa maelezo kuwa upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha pasi shaka yoyote mashitaka dhidi ya mwanaharakati huyo wa Kiislamu.
Wakati kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa, upande wa mashitaka uliita mashahidi wanane kwa lengo la kuthibitisha makosa dhidi ya Shehe Ponda ambaye alikuwa anatetewa na Mawakili wa kujitegemea Juma Nassoro na Abubakar Salum.
Shehe Ponda alifikishwa katika mahakama hiyo Agosti 19, 2013 akikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la kukaidi amri ya Mahakama ya Kisutu iliyomtaka awe mhubiri amani katika jamii likiwa ni sharti la kifungo cha mwaka mmoja nje baada ya kumtia hatiani katika kesi ya jinai.
Upande wa mashitaka ulidai kuwa Shehe Ponda alitenda kosa Agosti 10, 2013 katika eneo la Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege iliyoko katika Manispaa ya Morogoro.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo kiongozi huyo wa kidini alidaiwa kutoa maneno ya uchochezi ya kuhamasisha jamii kinyume na maelekezo ya mahakama.
Katika mkutano huo Shehe Ponda anadaiwa kusema maneno haya, “Ndugu Waislamu msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa CCM na Serikali na kama watajitokeza kwenu watu hao na kujitambulisha kwamba wao ni kamati za ulinzi na usalama za msikiti, fungeni milango na madirisha ya misikiti yenu na muwapige sana.”
Kauli hiyo inadaiwa kwenda kinyume cha amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es Salaam, iliyotolewa mahakamani hapo na Hakimu Victoria Nongwa, Mei 9, 2013 ambayo ilimtaka ndani ya mwaka mmoja kuhubiri amani na asifanye jambo lolote la uvunjifu wa amani na badala yake ahubiri suala la amani, ambayo ni kinyume cha Kifungu cha Sheria Namba 124 cha Mwaka 2002.
Shitaka la pili lililokuwa likimkabili Shehe Ponda ni uvunjifu wa sheria Kifungu cha 129 cha Makosa ya Jinai kuwa siku hiyo, alitoa maneno ya uchochezi yaliyohatarisha kuathiri imani za watu wengine.
Katika hati ya shitaka hilo, ilinukuu kauli ya Ponda kuwa “Serikali ilipeleka Jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi kwa kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Waislamu. Lakini Serikali haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo walipokataa Mwarabu asipewe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Wakristo.”
Shitaka la tatu anadaiwa kutenda kosa kinyume cha sheria kifungu cha 390 na 35 kwa kuchochea maneno dhidi ya wananchi wakati wa kongamano lililofanyika Agosti 10, 2013 Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege.


Jecha wa ZEC Atoka Mafichoni.....Dk. Shein Asisitiza Uchaguzi Lazima Urudiwe Zanzibar

Mpekuzi blog

Hatimaye  Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, jana ameonekana hadharani katika maadhimisho ya sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi zilizofanyika kwenye Uwanja wa Amaan mjini Unguja.

Jecha ambaye inaaminika alikuwa mafichoni tangu alipotangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar Oktoba 28, mwaka jana, alionekana ameketi kwenye jukwaa kuu la viongozi, jirani na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. John Magufuli na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

Kuonekana kwa Jecha hadharani kumezua mijadala mitaani na hata katika mitandao ya kijamii, huku wengi wakihoji alikuwa wapi mara baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi.

Watu mbalimbali wamekuwa wakihoji kuonekana kwa Jecha hadharani jana, siku ambayo Dk. Shein alitumia maadhimisho ya Mapinduzi kutangaza kwamba uchaguzi wa marudio Zanzibar iwe isiwe utafanyika.

Oktoba 28, mwaka jana majira ya saa sita mchana kwenye Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar zilizopo Kilimani mjini Unguja, ilikuwa ndiyo siku ya mwisho kuonekana Jecha hadharani.

Siku hiyo huku akiwa chini ya ulinzi wa vijana wawili wanaoaminika kuwa ni makomandoo wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania (JWTZ) waliovaa kiraia, Jecha alitangaza kuufuta uchaguzi wa Zanzibar mbele ya vyombo vichache vya habari.

Alitumia dakika mbili tu kuvitangazia vyombo hivyo vya habari juu ya adhima yake ya kuufuta uchaguzi na kutoa sababu zilizomfanya kufanya hivyo ikiwamo kuharibiwa kwa uchaguzi kisiwani Pemba.

Hata hivyo, baada ya kumaliza kutoa taarifa yake kwa vyombo hivyo, Jecha hakutaka kuulizwa maswali.

Oktoba 27, mwaka jana ikiwa ni siku moja kabla ya kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi, Jecha pia hakuonekana kwenye kituo cha kutangaza matokeo kilichokuwa katika Hoteli ya Bwawani kwa kile kilichodaiwa alipata matatizo ya kiafya na hivyo kumwachia kazi hiyo Makamu Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Abdulhakim Ameir Issa.

Siku hiyo majira ya saa kumi jioni, askari wa JWTZ walizingira kituo cha Bwawani na kuwaamuru watu waliokuwa ndani kutotoka nje na hata wale walioko nje ya kituo hicho kutosogea.

Watu waliokuwa ndani ya kituo hicho wengi wao walikuwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi pamoja na baadhi ya wawakilishi wa vyama vya siasa waliofika kusikiliza matokeo ya uchaguzi.

Dr. Shein asisitiza Uchaguzi lazima urudiwe
Kutokana na kile kinachoonekana kuendelea kupasuka kwa hali ya kisiasa visiwani Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesisitiza uchaguzi utarudiwa baada ya awali matokeo yake kufutwa na ZEC.

Akihutubia katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Uwanja wa Amaan jana, Dk. Shein alisema uchaguzi huo utarudiwa kwa mujibu wa katiba na sheria.

“Kila mmoja anajua kilichotokea katika uchaguzi Zanzibar baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi kutokana na kasoro zilizogundulika kutokea wakati wa uchaguzi huo,” alisema Dk. Shein na kuongeza:

“Suala la kurudiwa kwa uchaguzi liko palepale na utarudiwa kwa mujibu wa katiba na sheria, hivyo nawaomba wananchi muwe na uvumilivu na upendo wakati tukisubiri kutangazwa kwa tarehe ya kurudiwa uchaguzi.”

Licha ya kwamba kila upande umeshaweka msimamo wake, lakini Dk. Shein alisema mazungumzo ya kusaka suluhu yanaendelea baina ya pande hizo na kwamba taarifa ya mazungumzo hayo itatolewa punde yatakapokamilika.

“Tangu kutokea kwa mgogoro huu tulishauriana kukutana viongozi sita waliopo madarakani na waliostaafu ili kufanya mazungumzo ya kusaka suluhu na taarifa itatolewa pindi mazungumzo yatakapokamilika,” alisema Dk. Shein.

Tuesday, January 12, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya January 13

Mpekuzi blog

J

"Siasa za Hatari sana hizi, Siasa za kibaguzi. Siasa zinazopaswa kulaaniwa na kila mpinga ubaguzi nchini. Nitashangaa sana kama wakubwa CCM hamtaomba radhi kwa siasa hizi hizi mbaya kabisa. What will be the stop?"
By Zitto Kabwe

UNDP
EMPLOYMENT OPPORTUNITY

Visit HERE to Apply

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Afika Muhimbili Kumjulia Hali Waziri Mkuu Staafu Fredrick Sumaye

Mpekuzi blog
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Waziri Mkuu, Mstaafu Frederick Sumaye  ambaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu Januari 12, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amnaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa Matibabu Januari 12, 2016. Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Esther Sumaye.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Balozi Hassan 
Kibelloh ambaye naye  amelazwa katika hospitali ya taifa y Muhimbili kwa Matibabu Januari 12, 2016.

CM Yaomba Radhi Kutokana na Maneno ya Kibaguzi Kwenye Bango Katika Sherehe za Mapinduzi

Mpekuzi blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na mmoja wa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi.
Ujumbe huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na Mshikamano wa Kitaifa.
Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
12/01/2016

Monday, January 11, 2016

Shilole a.k.a Shishi Baby amesema baada ya kuachana na Nuh Mziwanda bado jimbo la moyo wake halijapata mgombea mpya wa kuziba nafasi yake.

Zimekuwepo tetesi kuwa Shishi anatoka na msanii mwingine wa Bongo fleva, Nyauloso zamani Bonge la nyau, huku wengine wakisema kuwa ana uhusiano na msanii wa Uganda, Eddy Kenzo.

Mimi sijapata mpenzi mpya mimi nipo tu, mpenzi mpya nitasema mwenyewe kwa mdomo wangu mimi,” Shishi ameeleza kupitia 255 ya XXL. “ nifanye interview niseme jamani sasa nina mpenzi mpya, lakini saizi msisikie rumors zinazotokea subirini mimi niwahakikishie.” Alisema Shishi.

Kuhusu Eddy Kenzo Shishi amedai kuwa ni kama kaka yake lakini wanawasiliana sana, na kuongeza kama endapo urafiki wao utazaa penzi basi atatangaza rasmi.

Baadhi ya benki nchini zinadaiwa kuajiri baadhi ya wafanyakazi walio kwenye mtandao wa majambazi kutokana na wateja wengi kupigwa risasi na kufa wakitoka kuchukua pesa, uchunguzi wa baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi Tanzania umebaini.

Hayo yalisemwa na baadhi ya askari hao wiki iliyopita walipozungumza na mwandishi wetu na kusema kwamba, waajiri wasipokuwa makini katika kuajiri watashangaa kuona wateja wao wanapigwa risasi na kuuawa kila kukicha.

“Haiwezekani kuwa wanaonyang’anywa fedha ni wale wanaotoka kuchukua benki kuliko wanaopeleka! Ina maana wezi wapo katika baadhi ya mabenki hivyo kunatakiwa kuwepo na umakini wakati wa kuwaajiri,” alisema askari mmoja kutoka makao makuu ya jeshi hilo, Dar akiomba hifadhi ya jina lake kwa vile yeye si msemaji.

Afande huyo aliendelea kusema kuwa, baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu wa benki hizo wanapoona mteja anachukua fedha nyingi hufanya mawasiliano kwa njia ya simu kuwaeleza majambazi walio nje namna alivyovaa mteja huyo na kiasi cha fedha alichochukua.
Uchunguzi zaidi unaonesha kuwa, endapo hali hiyo haitadhibitiwa haraka huenda wananchi wakapatwa na hofu ya kuweka fedha zao benki kwa kuogopa kuporwa na kupigwa risasi wakienda kuzichukua.

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Simon Sirro (pichani) ambapo alikiri kuwepo kwa baadhi ya wafanyakazi wenye mtandao na majambazi huku akisema jeshi lake limeweka mikakati kuhakikisha mtandao huo unasambaratishwa mara moja.
“Ni kweli kwamba, baadhi ya mabenki, si yote, yameajiri baadhi ya wafanyakazi, si wote wenye mtandao na majambazi. Kwa hiyo hata wao ni majambazi tu.

“Sasa tumejipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kukamata pikipiki zinazohusika katika uhalifu. Pia tumeamua kuweka makachero nje na ndani ya mabenki, wapo polisi wa miguu, pikip iki na magari. Nina uhakika tutawadhibiti,” alisema Kamanda Sirro.

Aliendelea kusema kuwa, majambazi waliopo katika Kanda ya Dar es Salaam waanze kufunga virago kwani bila kufanya hivyo wajue watakamatwa wote na mtandao wao kumalizika. Pia aliwataka wamiliki wa mabenki kuwa makini wakati wa kuajiri wafanyakazi ili kuwapata wenye sifa njema na kuweka imani kwa wateja wao.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova aliwahi kutamka kuwa, baadhi ya wafanyakazi wa ndani wa baadhi ya benki wana ushirikiano na majambazi. Akawatahadharisha wamiliki kuwa makini wakati wa kuajiri.

HAYA ni mazito! Nyuma ya shughuli ya kuolewa kwa staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma na Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma iliyofungwa Alhamisi iliyopita, kuna matukio ya kustaajabisha ambayo Ijumaa Wikienda limeyabaini.

Ndoa hiyo iliyofungwa kimyakimya, ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa mwigizaji huyo, Tabata-Barakuda, jijini Dar ambapo ilihudhuriwa na watu wachache tofauti na ilivyotarajiwa kutokana na umaarufu wa wanandoa hao.

NDOA ILIFUNGWA KWA SIMU
Imebainika kuwa, awali ndoa hiyo ilikuwa ifungwe saa kumi jioni na baadaye kuelezwa ilisogezwa mbele hadi saa 12 jioni, hata hivyo haikufungwa muda huo baada ya bibi harusi kuchelewa kufika akitokea saluni alikoenda kupambwa na kulazimika shehe afungishe ndoa hiyo kwenye simu wakati Wastara akiwa kwenye foleni barabarani.

BWANA HARUSI AGOMA KUPIGWA PICHA
Imeelezwa kuwa, baada ya bwana harusi kutinga na wapambe wake alitoa onyo kali huku likisisitizwa na wapambe wake kuwa hairuhusiwi kupiga picha na kutuma kwenye mtandao wowote wa kijamii kwa vile ndoa hiyo ilikuwa ya siri.

AGOMA KUMFUNUA BIBI HARUSI
Katika hali ya kushangaza, baada ya bibi harusi kuwasili aliingizwa katika chumba maalum kwa ajili ya kumsubiri mumewe na hata alipoingia ndani, shehe alimuomba amfunue mkewe ili kumhakikisha kama ndiye yeye kitu ambacho alikipinga na kudai hakuwa na shaka naye na kuomba waendelee na kitu kingine.

WASTARA ASHINDWA KUPATA MSOSI
Jambo lingine ambalo lilizua minong’ono ni Wastara kushindwa kupata muda wa kula chakula ambacho kiliandaliwa kwa sababu baada ya kumaliza kupiga picha za familia na kushikana mkono na mumewe, mumewe alimtaka waondoke huku akimwambia dereva wao awashe gari.

WADOGO WA SAJUKI WALIA
Katika hali ambayo haikuweza kufahamika mara moja, wadogo wa aliyekuwa mumewe wa pili wa Wastara, merehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Mohamed Kilowoko na Njegere Kilowoko waliangulia kilio kwa kile walichodai walikuwa na huzuni na furaha.