WALIOTUHUMIWA MAMLUKI CHADEMA WAVULIWA UONGOZI.
Na Bryceson Mathias, Kilosa.
NGUVU ya Umma ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya
Ruaha, Jimbo la Mikumi, Wilaya ya Kilosa, Morogoro, wamewavua Uongozi
waliokuwa Viongozi wao na kuweka Kamati ya Muda (Task Force), kwa madai
ya kuwa Mamluki ndani ya Chama chao.
Waliovuliwa Uongozi na kubaki na Uanachama ni pamoja na aliyekuwa
Mwenyekiti wa Kata, George Banda, Katibu, Ally Mponda, Katibu Mwenezi,
William Temu, Mweka Hazina, Aurelia Mnunga, na Mjumbe wa Kamati
Tendaji, Mwalimu Myami.
Katika Kikao cha ndani cha Julai 2 (Ukumbi wa Linas), kilichosimamiwa na
Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mafunzo wa Chadema Taifa, Benson Kigaila;
Baada ya kusikiliza ‘Tuhuma’ za Viongozi hao, aliwauliza wanachama
wanataka nini, ambapo wote walipaza Sauti; Wavuliwe Uongozi na kubaki
Wanachama!.
Aidha Tuhuma zilizoelekezwa kwa Viongozi hao, ni Kuwafukuza Viongozi
wenzao Watatu wa Chadema, kwa kutumia Vifungu visivyokuwemo kwenye
Katiba ya Chadema, ilihali wakijua ni kukinyang’anya Chadema Ushindi
wake halali na kukifurahisha Chama Mapinduzi(CCM).
Nyingine ni Viongozi hao kuhamisha Vikao vya Chama, ambapo badala ya
kufanyia kwenye Ofisi ya Chadema Kata, kwa Miezi zaidi ya Minne
walihamishia Vikao na Ofisi kwenye Mgahawa wa mmoja wa Viongozi hao
kinyume cha Katiba.
Kiongozi Mpya, Abasi Longa, alikiri kuchaguliwa Mwenyekiti wa Muda kati
ya Viongozi waliochaguliwa na Wanachama; Hii ikiwa ni mara tu baada ya
kumvua, Banda aliyekuwa Mwenyekiti, ambapo, Joram Zacharia,
alithibitisha kuchukua UKatibu aliovuliwa, Mponda.
Mbali ya waliovuliwa nyadhifa kutotaka kuzungumza na Mwandishi hata
walipopigiwa simu za Viganjani kuelezea walivypokea kuvuliwa Uongozi na
kuwa Wananchama; Aliyekuwa Katibu, Mponda, pekee alikiri kuondolewa,
akisema, “Siasa ni Kijiti, lazima tupokezana”.alisema
Hata hivyo, Longa alikiri kupokea Fomu za Viongozi watatu waliovuliwa
Uongozi na kubaki Wanachama wa Chadema, Banda, Mponda na Mnunga, ambao
wametia nia ya Udiwani wa Kata hiyo.
Awali Mponda, alimthibitia Mwandishi wa habari, kuhusu azma yake kutia
nia ya kugombea Udiwani wa Kata hiyo wakiwemo Viongozi wenzake
waliovulia Madaraka, jambo ambalo limeendelea kuwawatia Shaka Wana
Chadema kuwa, huenda kulikuwa na kitu nyuma ya Pazia
No comments:
Post a Comment