Mafuriko Ya Lowassa Yatua Jijini Dar......Kingunge Amwaga Wino Hadharani Kumdhamini, WanaCCM 212,150 Wajitokeza Kumdhamini
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa amepata udhamini wa kishindo katika mkutano uliofanyika jana katika ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni.
Lowassa alipata udhamini huo baada ya wanachama kujitokeza katika
ofisi za Makao Makuu ya CCM ya Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni, Dar,
ambapo alipata zaidi ya wadhamini 212,150 huku akisema Dar imevunja rekodi ya mikoa
yote ya Tanzania.
Akizungumza
na maelfu ya wananchi waliofika katika mkutano huo
Lowassa alisema kuwa amefurahishwa na watu waliojitokeza kumdhamini kwa
kishindo kikubwa na hivyo hatavunjwa moyo na maneno ya watu
yanayovumishwa kuwa anawapatia fedha ili wafike kwenye mkutano wake .
Lowassa aliongeza kuwa anawaomba Watanzania wampe ridhaa ya kuwa rais wao
kwani atahakikisha mianya yote ya rushwa na utendaji mbovu wa kusuasua
anausimamia kwa haki na weredi na ndani ya miezi sita tayari matokeo
yatakuwa yameonekana.
“Nawaombeni wananchi mnipeni ridhaa ya kuingia ikulu yaani
nitahakikisha mianya yote ya rushwa na ufisadi nautokomeza, muyapuuze
maneno na minong’ono ya watu kutaka kunichafua,” alisema.
Mwanasiasa
Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisani fomu ya
udhamini mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward
Lowassa ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono mgombea huyo.
Zoezi
hili lilifanyika jana jioni ya Juni 27, 2015 kwenye Ofisi za CCM Wilaya
ya Kinondoni, Mkwajuni Jijini Dar ambapo Lowassa alipata jumla ya
Wadhamni 212, 150 na kuifanya Dar es salaam kuwa Mkoa wa kwanza kuwa na
idadi kubwa ya WanaCCM waliomdhamini .
No comments:
Post a Comment