Wolper: Mimi ni Freemason Kitambo tu
Mtoto mzuri katika tasnia ya uigizaji Bongo, Jacqueline Wolper Massawe ‘Twiga wa Jangwani’ amesema haoni sababu ya kuukana uanachama wa taasisi ya Wajenzi Huru (Freemason) kwani ni dini kama zilivyo zingine na kama katiba inavyoelekeza, kila mtu anayo haki ya kujiunga na dini au taasisi yoyote ya kuabudu kulingana na matakwa ya imani yake.
Akiongea na mwandishi wetu, Wolper alisema ni kweli
yuko katika kundi hilo huku akishangaa watu kustaajabu kuona mtu yuko
Freemason wakati walioanzisha dini hiyo ni binadamu kama wengine.
“Freemason si ni taasisi au dini kama zingine? Kuna ajabu gani mimi
kuwa mwanachama? Tena nataka nikuhahakikishie kuwa, nimekuwa muumini
halisi wa Freemason kwa muda mrefu sasa,” alisema Wolper.
No comments:
Post a Comment