Lowassa: Magufuli Anatekeleza Hoja Zangu na Chadema
Mpekuzi blog
Aliyekuwa
mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema kuwa
serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Magufuli imeanza
kuzifanyia kazi hoja zake alizozieleza wakati wa uchaguzi.
Lowassa
aliyasema hayo jana jijini Arusha alipokuwa akimnadi mgombea ubunge wa
jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema katika uwanja wa shule ya msingi
Sinoni.
Lowassa
aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kumuachia huru Sheikh Issa
Ponda na kuiomba kuliangalia pia suala la mwanamuziki, Nguza Vicky (Babu
Saye) na mwanae.
“Haya
mambo ndiyo tuliyoyaema wakati wa kampeni, sasa namuona Magufuli
ameanza kuyatekeleza. Sasa nawaomba angalau wawe wanasema hizo ni sera
za Lowassa na Chadema na wanapozitumia basi wawe wanatushukuru,” alisema
Lowassa.
Kauli
hiyo ya Lowassa iliungwa mkono na waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye
ambaye aliwataka pia wananchi wa jimbo hilo kumchagua Lema ili aende
bungeni akatumbue majipu ambayo yanapeleka damu kwenye mishipa ya moyo,
majipu ambayo alidai CCM haiwezi kuyatumbua.
No comments:
Post a Comment