Mhindi Aliyekamatwa na Milioni 700 Dodoma Arudishiwa Fedha zake
Jeshi la polisi mkoani Dodoma limekanusha taarifa zilizozagaa kuhusiana na Raia wa Asia kukamtwa na fedha zaidi ya sh. m.700 kwa madai ya kuwahonga wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM ili wamchague mmoja kati ya waliokuwa wanawania nafasi ya Urais
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari na kamanda wa
polisi mkoani hapa, David Misime mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Amit
Kevalramani aliyekamatwa juma lililopita kwenye hoteli ya St Gaspar
mjini hapa ni mganyabiashara wa mazao ya nafaka ni siyo mpambe wa
wanachama wa CCM waliokuwa wanawania Urais.
Misime
amesema mnamo siku ya Julai 11 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi kuna
baadhi ya wananchi walitoa taarifa kwa jeshi la polisi kwamba kuna mtu
mmoja mwenye asili ya Kiasia amekamatwa na wananchi akiwa na fedha
nyingi na kuna vurugu kubwa katika hotel ya St Gaspar.
“Baada
ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi mkoani hapa lilifika eneo la
tukio ili kuona kama taarifa hizo ni za kweli, askari walithibitisha
kuwa ni kweli, walimkuta mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia ambaye
alijulikana kwa jina la Amit Kevalramani (31), Mhindi, Mfanyabiashara,
Mkazi wa Dar es Salaam akiwa na fedha kiasi cha sh. 722 milion ambacho
alipohojiwa alisema kuwa Julai 10 mwaka huu alifika Dodoma kwa ajili ya
ununuzi wa mazao ya nafaka” amesema Misime na kuongeza;
“Alipofika Dodoma hiyo siku majira ya asubuhi alifikia katika Hoteli ya St. Gasper na kesho yake Julai 12 aliamua kurudisha fedha benki kutokana na kuona mkusanyiko wa watu wengi wasioeleweka na wenye viashiria vya vurugu.”
“Alipofika Dodoma hiyo siku majira ya asubuhi alifikia katika Hoteli ya St. Gasper na kesho yake Julai 12 aliamua kurudisha fedha benki kutokana na kuona mkusanyiko wa watu wengi wasioeleweka na wenye viashiria vya vurugu.”
Misime
alisema kuwa akiwa katika harakati ya kurejesha fedha hizo benki, ndipo
kundi la watu waliokuwa katika eneo la Hoteli hiyo ya St. Gaspar
walimtilia mashaka na kumzuia asiondoke na ndipo taarifa zilitolewa
polisi.
Alisema
mashaka ya watu hao yalitokana na vuguvugu za kisiasa na mchakato wa
uchaguzi kati ya makundi mbalimbali kuwa kuna watu wanahonga wajumbe.
Taarifa za aina hiyo ambazo hata Jeshi la Polisi lilikuwa limepokea bila
uthibitisho.
Alibainisha
kuwa uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi umebaini kuwa hakuna kosa
la jinai lililothibitika licha ya kukutwa na kiasi hicho cha fedha,
tuhuma za rushwa ambazo ndiyo zilikuwa msingi wa ukamataji wa mtu huyo
hazikuthibitika, kwa kuwa hakuna aliyeona akizigawa fedha hizo wala
hakuna aliyedai kushawishiwa au kugawiwa fedha hizo.
Aidha
imethibitika fedha hizo ni mali yake halali na kwa kuwa hakuna ushahidi
mwingine uliyo thibitisha vinginevyo amerejeshewa fedha zake.
Wakati
huo huo kamanda amesema kuwa mnamo Julai 10 mwaka huu majira ya saa
21:00 eneo la Railway Dodoma jeshi la polisi lilifanikiwa kuwakamata:-
1. HERERIMANA METHODE, MIAKA 21.
2. HATUNGIMANA ALEXIS, MIAKA 20.
3. NIYONGABO JUSTIN, MIAKA 20.
4. NTETURUYE ONESPHORE MIAKA 21.
5. BIKORIMANA LEVIS, MIAKA 21 wote ni Wakazi wa Mabanda Burundi kwa kosa la kuingia nchini na kuishi nchini bila kibali.
Watuhumiwa
hawa walikuwa wanasafiri na treni kuelekea Dar es Salaam na walipofika
Dodoma Askari wanaosindikiza treni waliwashtukia na walipowakamata na
kuwahoji walijieleza kuwa ni raia wa Burundi.
Tunaomba
ushirikiano wa wananchi pale wanapoona watu ambao siyo raia
wasiwakaribishe bali watoe taarifa kwa vyombo vya dola waweze kuhojiwa
kwani hata kama waliingia Nchini na kuhifadhiwa katika makambi yaliyopo
Nchini hawaruhusiwi kutoka kwenda mbali na kambi zao bila kuwa na kibali
maalum.
No comments:
Post a Comment