Wednesday, July 15, 2015

Atakayewataja Watu Walioteka Kituo na Kuua Polisi Atapewa zawadi ya Milioni 50


Jeshi la polisi nchini  Tanzania limetangaza kutoa zawadi  ya shilingi za kitanzania million 50 kwa mtu yeyote mwenye taarifa za uhakika na za haraka zitakazofanikisha kuwakamata wote waliovamia kituo cha polisi stakishari na kuua askari na raia waliokuwa katika kituo hicho usiku wa kuamkia jana.
 
Akitoa tarifa mbele ya wanahabari  kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleimani  Kova  amesema kuwa kupitia dhana ya polisi ya ulinzi shirikishi mkuu wa jeshi la polisi IGP  Ernest Mangu ameona ni muhimu kuwashirikisha wananchi kikamilifu katika suala hili linalohusiana na ulinzi na usalama wao na watanzania wote kwa ujumla.
 
Jeshi hilo limesema kwamba  Mtu yeyote atakaye atakayefanikisha kukamatwa ikiwemo  kutoa taarifa sahihi  kwa viongozi wakuu wa jeshi la polisi atajipatia zawadi hiyo bila hiyana.
 
Namba za kupiga kama unazo taarifa sahihi ni hizi zifuatazo;
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM (CPS.H KOVA) —–0754034224
 
MSEMAJI WA JUESHI LA POLISI (SSP ADVERA BULIMBA)—–0713631667
 
MKURUGENZI WA MAKOSA YA JINAI (CP DIWANI ATHMAN)—-0715323444
 
Aidha wananchi wenye taarifa husika pia wanaweza kuonana uso nkwa uso na viongozi wakuu wa makao makuu ya polisi au kanda maalum na kuwapa taarifa moja kwa moja
 
Jeshi  hilo  limesisitiza kuwa   mwananchi ambaye ataleta taarifa husika na kufanikisha zoezi hilo itakuwa  siri kubwa na hatajulikana popote kama yeye ndiye mtoa taarifa husika.

No comments:

Post a Comment