Rais Dkt. Jakaya Kikwete awatunuku Nishani watumishi wa umma walioliletea sifa Taifa
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimvisha
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro Nishani ya Jamhuri ya Muungano
Daraja la Kwanza kwa kuwa mwaminifu na kujitolea moja kwa moja kulipatia
Taifa sifa kubwa katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiulinzi na
kijamii wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu
leo Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akimvisha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Liberata Rutegaruka Mulamula Nishani ya Jamhuri ya Muungano Daraja la
Kwanza kwa kuwa mwaminifu na kujitolea moja kwa moja kulipatia Taifa
sifa kubwa katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiulinzi na kijamii
wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu leo
Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akimvisha
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Martin Turuka Nishani
ya Utumishi mrefu na Maadili mema Daraja la kwanza kwa kuwa mtumishi wa
umma kuanzia ngazi ya ukurugenzi na kutumikia Taifa si chini ya ishirini
mfululizo na kuonyesha maadili mema wakati wa sherehe zilizofanyika
kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akimvisha
akimvisha Balozi wa Tanzania nchini Burundi Rajabu Hassan Gamaha
Nishani ya Utumishi mrefu na Maadili mema Daraja la kwanza kwa kuwa
mtumishi wa umma kuanzia ngazi ya ukurugenzi na kutumikia Taifa si chini
ya ishirini mfululizo na kuonyesha maadili mema, wakati wa sherehe
zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.
Mwalimu
Rosalia Marmo Massay akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete baada ya kuvishwa nishani ya
Utumishi mrefu na maadili mema Daraja la Pili kwa kufanya kazi bora na
maadili mema yanayostahili kuigwa na wengine kwa muda usiopungua miaka
ishirini wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu
leo Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akimvisha
CPL Liberatus Tibaitirwa Ndyetabula nishani ya Ushupavu inayotolewa kwa
majeshi ya ulinzi na Usalama na watu wengine kwa vitendo vya ushupavu,
wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu leo
Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi waliovishwa nishani
mbalimbali leo Jijini Dar es salaam.Kushoto ni Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman na kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
Mtoto huyo akimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete picha aliyoipiga.
Mtoto
wa Mmoja ya viongozi waliovishwa nishani akipiga picha ya pamoja
iliyomjumuisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Mrisho kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi
waliovishwa nishani
………………………………………………………………………..
Na Hassan Silayo
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo
amewavisha nishani mbalimbali watumishi wa Serikali kwa kutambua mchango
wao kitaifa.
Rais
Kikwete amefanya hivyo kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya sheria
ya mamlaka ya Rais (sura ya 9) kamailivyorekebishwa mwaka 2002 fungu la 4
kama ilivyotangazwa katika tangazo la serikali namba 227.
Nishani
zilizotunukiwa leo ni Nishani ya Jamhuri ya muungano Daraja la Kwanza,
Nishani ya Utumishi mrefu na Maadili mema Daraja la kwanza, Nishani ya
utumishi mrefu na Maadili mema Daraja la pili na Nishani ya Ushupavu.
Nishani hizo zinatunukiwa kwa watumishi ambao sifa zao zimekidhi mmatakwa ya nishani husika
No comments:
Post a Comment