Thursday, June 4, 2015

Nyalandu kuhutubia wananchi Singida, akijitayarisha kuchukua fomu

Tarehe June 4, 2015
Waziri  wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Waziri  wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu anatarajia kufanya mkutano wa hadhara mkoani Singida mwishoni mwa wiki akijitayarisha kwenda makao makuu ya CCM kuchukua fomu ya kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi juni 8.
Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa  kwa waandishi wa Habari  Nyalandu amebainisha kuwa  baada ya kuhutubia mkutano wake huo wa hadhara, atakwenda mjini Dodoma kuchukua rasmi fomu ya urais siku ya Jumatatu, Juni 8.
Nyalandu  ni mmoja wa mawaziri watakao ungana na wenzake akiwemo John Magufuri, Steven Wassira Mark Mwandosya   katika Serikali ya awamu ya nne ambao wanataka ridhaa ya chama cha Mapinduzi kuteuliwa kugombea urais mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment