Sunday, June 7, 2015

Mbinu nyingine iliyotumiwa na wanawake hawa kusafirisha dawa za kulevya Nigeria !!

Uzoma Alaka and Priscilla Chukwujekwu
Wanawake waliokamatwa na dawa za kulevya Nigeria, Uzoma Alaka na Priscilla Chukwujekwu.
Headlines nyingine kwenye vyombo vya habari ni ishu ya dawa za kulevya… China ni moja ya nchi ambazo kwa Sheria zao ikitokea umekamatwa na dawa za kulevya, hukumu yake ni kunyongwa, lakini bado wapo wanaoingia kwenye nchi hiyo kwa biashara hiyo hiyo ya dawa za kulevya.
Nimekutana na hii toka Lagos Nigeria, wanawake wawili wamekamatwa na dawa za kulevya aina ya cocaine zenye uzito wa kilo 2.5… mbinu waliyotumia wao ni kuweka dawa hizo sehemu za siri na nyingine walimeza, walikamatwa Uwanja wa Ndege na safari yao ilikuwa waingie China!!
Ni hukohuko Nigeria aliwahi kukamatwa jamaa ambae alikuwa anasafirisha dawa za kulevya ndani ya viatu, hii ni mbinu yao nyingine ambao imechukua headlines kubwa mitandaoni.

No comments:

Post a Comment