Zari Tlale aka The Bosslady amesema upendo anaoupata baada ya kuanzisha
uhusiano na Diamond Platnumz, umemfanya agundue kuwa watanzania
wamemkubali kama mtu wao.
Akiongea na Clouds FM/TV asubuhi hii, Zari amesema tangu ameanza kuja
Tanzania amekuwa akipokea upendo zaidi kutoka kwa watanzania kiasi
ambacho kimemfanya ajisikie kama yupo kwao.
“Siwezi hata kulalamika, watu wa Tanzania ni wakarimu sana ni watu
wazuri sana, kwangu mimi sijapata hata tatizo, siwezi hata kusema kitu
chochote kibaya kuhusu watu wa Tanzania,” alisema.
“Wamenikaribisha kama ni mtu wao na sasa mimi ni wao hivyo ni yote ni heri kabisa,” aliongeza.
Katika hatua nyingine Zari amesema Tanzania itageuka kuwa makazi yake ya
mara kwa mara na mipango iliyopo ni kuanzisha mradi wa kibiashara
nchini lakini baada ya kufanya utafiti na kubaini fursa za uhakika.
“Siwezi tu nikafungua biashara hapa eti kwasababu mimi ni maarufu
nikafungua tu biashara ya kijinga na nikidhani ninaweza nikauza wazo
langu la kijinga kwa watu hapa, wao sio wajinga wanatumia hela zao hivyo
nahitaji kubaini wapi kuna hitaji, kipi naweza kufanya na hapo ndipo
ntaenda na kuwekeza fedha zangu.”
posted by rashid
No comments:
Post a Comment