KIGOMA - Tanzania Entertainment News,Politics News ...
kigoma tunaamini sisi sote ni wazalendo wa ukweli basi pata habari zote hapa kwa blog yetu muhimu na pendwa kwa mkoa wa KIGOMA - TANZANIA ENTERTAINMENT News,Politics and other basi unguna na kijana mwenzako RASHID HAMZA MAARUFU KWA JINA LA RD PRO DOGO 'R' SIMU NAMBA 0752987701 PAMOJA TUNAJENGA NCHI YETU NA TUTASHINDA
Tuesday, November 28, 2017
Friday, November 24, 2017
Kafulila atua rasmi CCM na Kukabidhiwa Kadi
Baada ya kutangaza kujivua uanachama wa CHADEMA siku ya Jumatano, David Kafulila jana amekabidhiwa kadi ya CCM.
Kafulila
alikabidhiwa kadi ya CCM na Katibu Mwenezi wa CCM, ndg Humphrey
Polepole katika mkutano wa kumnadi mgombea wa udiwani wa chama hicho,
Kata ya Mbweni jijini Dar es salaam
Hapo
awali Kafulila aliwahi kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na
Maendelo kisha kufuzwa baadae akajiunga na Chama cha NCCR Mageuzi ambapo
alifanikiwa kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini mwaka 2010-2015 na baadaye
kurudi tena Chadema 2016 na hapo juzi jumatano alitangaza kukihama chama
hicho kwa madai upinzani hauna nia ya kupambana na ufisadi.
Kwa
upande wa mkewe ambaye ni Mbunge Viti Maalumu kupitia chama cha
CHADEMA,Jesca Kishoa juzi wakati akizungumza na wanahabari alipingana na
kauli ya mumewe na kusema kwamba, mumewe anapaswa kusema ukweli na
kwamba sababu alizozisema sizo zilizomuondoa ndani ya chama hicho huku
akiongeza kwamba mume wake hana msimamo.
Kafulila
amekabidhiwa kadi hiyo ya CCM ikiwa imebaki siku moja kabla ya
kuhitimishwa kwa kampeni za uchaguzi wa marudio ya nafasi za udiwani kwa
Kata 43 ndani ya Tanzania
Thursday, November 23, 2017
Breaking News: TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia
Mchambuzi Huru imepata uthibitisho wa taarifa za kifo cha Mhe. Gama ambacho kinadaiwa kutokea muda wa Saa 6 kuelekea Saa 7 usiku wa kuamkia leo.Amefariki akiwa mbunge wa Songea Mjini na amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii Songea katika Hospitali ya Peramiho.
Gama amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.
Inadaiwa marehemu Gama alianguka nyumbani kwake saa saba usiku juzi huko Likuyu; akapooza upande wa kushoto akawa hajitambui kabisa na akapelekwa Hospitali ya Peramiho ambako aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi
Mke wa Kafulila Atoa ya Moyoni Uamuzi wa Mumewe Kuikimbia CHADEMA
Mke wa aliyewahi kuwa mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, Jesca Kishoa, amemtaja mumewe kuwa ni mtu aliyeingia kundi la wanasiasa wasio na msimamo.Kishoya amesema wakati wote mumewe amekuwa na msimamo usioyumba lakini anashangazwa kaingia katika mtego mbovu.
"Bado naamini kuwa Chadema ni mahali sahihi kabisa ambapo siwezi kufikiri siku moja nitatoka, hivyo siyumbi kwa hilo na wanaonipigia simu watambue hilo," amesema Kishoya
Amesema taarifa za mumewe kujiondoa Chadema amezipata kupitia vyombo vya habari akiwa Dodoma kwenye kampeni za udiwani lakini alimpigia wakazungumza sana na bado hakumpa sababu zilizoshiba za kuondoka kwake.
Hata hivyo amepinga madai ya Kafulila kuwa anaondoka upinzani kwa sababu ya upinzani kushindwa kusimamia ajenda ya ufisadi badala yake akasema ana mambo yake.
"Wanasiasa ambao hawana misimamo ndiyo husingizia vitu hivyo, siamini kama maneno yale yalitoka rohoni mwake, CCM siyo mahali sahihi kwa kuzungumzia mambo ya ufisadi hata kidogo, "
Mbuge huyo amesema wakati wote katika maisha yao mumewe amekuwa ni muumini mzuri wa kuhubiri habari za ufisadi ikiwemo pale alipotoa maisha yake kuhusu sakata la Escrow.
Kafulila: "Ndoa Yangu Haihusiani na Siasa ilifungwa Kanisani na Sio kwa Mwenyekiti wa Chama"
David Kafulila ambaye hapo jana amekihama chama cha CHADEMA, amesema suala la mke wake kuridhia au kutoridhia kwa yeye kuhama chama wakati yeye ni Mbunge wa chama hiko, ni suala ambalo halihusiani na ndoa yao.Kafulila ameyasema hayo leo na kueleza kwamba linapokuja suala la ndoa hapo ndio huwa lazima wafikie makubaliano, lakini ikija suala la kisiasa kila mtu ana uamuzi wake ambao hawaingiliani kwani ndoa yao ilifngwa kanisani na sio kwenye chama.
“Haya ni maamuzi ya kisisasa, sisi ndoa yetu ilifungwa kanisani haikufungwa kwa mwenyekiti wa chama au kwenye chama, kwa hiyo ndoa ni jambo jingine na harakati ni mjambo jingine, yeye ni mke wangu lakini haimaanishi tunakubaliana kwenye kila kitu, tunakubaliana kwenye mambo ya ndoa, kwenye siasa kila mtu anaweza akatazama jinsi anavyotazama yeye na sio shida”, amesema Kafulila.
Hivi sasa kumekuwa na mvutano kati ya wanandoa hao baada ya Kafulila kuhama CHADEMA, huku mke wake akisema hakuwa na taarifa zozote, na hata hizo sababu zake za kuhama hazina ukweli na kumtaka aweke wazi sababu rasmi za kufanya hivyo
Subscribe to:
Posts (Atom)