MCHEZAJI KANU WA NIGERIA AZINDUA DUKA JIPYA LA STARTIMES,LEO KWENDA KUTEMBELEA SHULE YA MSINGI MAJIMATITU MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM
Mchezaji
nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza,
Nwankwo Kanu (kulia),akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka
la Kampuni ya StarTimes lililopo jengo la Mkuki Mall Barabara ya
Nyerere Dar es Salaam leo mchana. Mchezaji huyo yupo nchini kwa ziara ya
siku tano. Kulia kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao.
Ofisa Mauzo wa StarTimes Tanzania na
mshereheshaji wa uzinduzi huo, Tang Jing Yu 'Juma Shorabaro wa Kichina'
(kulia), akiendelea na majukumu yake.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Mr.Canter, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao (wa pili kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkutano ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au
Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaamleo
mchana, baada ya kuzindua duka la Kampuni ya StarTimes lililopo jengo la
Mkuki Mall wakati wa ziara yake aliyoianza jana nchini. Kutoka kulia
ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Mr.Canter, Ofisa
Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao, Katibu wa mchezaji
huyo, Kingstey Obiekwe na Makamu wa Rais wa StarTimes, Zuhura Hanif.
Mchezaji
nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza,
Nwankwo Kanu (katikati), akitia saini yake katika jezi.
Kanu akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa StarTimes na wa jengo la Mkuki Mall baada ya kuzindua duka hilo.
Mmiliki wa Blog ya Full Shangwe, John Bukuku akichukua picha na mchezaji huyo.Na Dotto Mwaibale
Aliyekuwa
mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Naijeria (Super Eagles) na Arsenal ya
Uingereza, Nwankwo Kanu ameshiriki katika uzinduzi wa duka jipya la
kampuni ya StarTimes Tanzania lililopo katika jengo la Mkuki Mall
Barabara ya jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo mchezaji Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa
makampuni ya StarTimes barani Afrika ambapo inafanya shughuli zake
katika nchi zaidi ya 10 amesema kuwa anajisikia mwenye furaha kuwepo
nchini na atashiriki shughuli mbalimbali za kampuni pamoja na za
kijamii.
“Ni mara ya
kwanza mimi kuwepo nchini Tanzania, nashukuru nimefika salama na
kupokelewa kwa ukarimu mkubwa, kwa kweli sikutarajia. Uwepo wangu hapa
ninaiwakalisha kampuni ya StarTimes barani Afrika kama balozi wao na
kama balozi ninao wajibu wa kufika kila nchi ambayo kampuni hii ipo. Kwa
namna nilivyopokelewa ninaamini kuwa kweli StarTimes ni kampuni kubwa,
inapendwa na kujulikana miongoni mwa watanzania wote.” Alielezea Bw.
Kanu
“StarTimes
wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kuwa wateja wake wote
wanafurahia huduma za matangazo ya dijitali kwa ubora wa hali ya juu na
gharama nafuu. Na hii ni kutokana na falsafa iliyojiwekea kampuni ya
kutaka kuhakikisha kuwa kila nyumba ya muafrika inafikiwa na matangazo
hayo. Changamoto ni nyingi katika uendeshaji na utoaji huduma za
kidijitali lakini kampuni imejizatiti kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika
uboreshaji wa vipindi na chaneli zake. Kwa mfano kwa sasa kama
mnavyoweza kushuhudia kuwa ligi kubwa barani Ulaya za Bundesliga na
Serie A za nchini Ujerumani na Italia zinaonyeshwa moja kwa moja kupitia
StarTimes Pekee.” Aliongezea Kanu
“Michezo na
burudani ni maudhui muhimu sana ambayo lazima yawekewe mkazo kwani
ndivyo vitu vinavyopendwa na kuwavutia wateja wengi hivyo haina budi
kuweka mkazo. Ninaamini kuwa uwepo wangu nchini Tanzania utasaidia kwa
kukaa chini na uongozi wa kampuni nchini na kuweza kuona wanawaongezea
na kuwapatia nini wateja wao. Ninatumaini ninacho cha kuongezea kwa
nilichojifunza kutoka nchi kama za Uganda na Kenya ambazo nimetokea huko
pia,” alisema na kumalizia Kanu kuwa, “Nashukuru kuwepo Tanzania na
ninaamini nitajifunza na kushirikiana kwa mengi kwa kipindi
nitakachokuwepo mpaka kuondoka kwangu.”
Naye kwa upande
wake akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya ambalo litakuwa
ni la saba kwa mkoa wa Dar es Salaam pekee, Mkurugenzi wa Uendeshaji
(Operesheni) wa StarTimes Tanzania, Bw. Carter amebainisha kuwa duka
hilo jipya litawarahishia wateja wote wanao kama maeneo ya jirani kama
vile Tandika, Mbagala, Temeke, Kurasini, Yombo, Kiwalani, Vingunguti na
kwengineko kujipatia huduma na bidhaa kwa urahisi zaidi.
“Leo tunayo
furaha kubwa kufungua duka hili jipya ambalo katika kumbukumbu litakuwa
limezinduliwa na balozi wetu barani Afrika, Nwanko Kanu. Duka hili
litakuwa msaada mkubwa kwa wateja walio maeneo ya jirani na kwingineko
na ningependa kuwatoa wasiwasi kuwa litakuwa linatoa huduma zenye ubora
sawa na maduka yetu yote hivyo wasiwe na wasiwasi. Ninawaomba wateja
wetu watembelee hapa kujipatia huduma kama vile kununua visimbuzi,
antena na kebo, vocha za malipo ya mwezi pamoja na huduma kwa wateja.”
Alimalizia Bw. Carter.
No comments:
Post a Comment