Atakayewataja Watu Walioteka Kituo na Kuua Polisi Atapewa zawadi ya Milioni 50
Jeshi la polisi nchini Tanzania limetangaza kutoa zawadi ya shilingi za kitanzania million 50 kwa mtu yeyote mwenye taarifa za uhakika na za haraka zitakazofanikisha kuwakamata wote waliovamia kituo cha polisi stakishari na kuua askari na raia waliokuwa katika kituo hicho usiku wa kuamkia jana.
Akitoa tarifa mbele ya wanahabari  kamishna wa polisi kanda maalum ya
 Dar es Salaam Suleimani  Kova  amesema kuwa kupitia dhana ya polisi ya 
ulinzi shirikishi mkuu wa jeshi la polisi IGP  Ernest Mangu ameona ni 
muhimu kuwashirikisha wananchi kikamilifu katika suala hili 
linalohusiana na ulinzi na usalama wao na watanzania wote kwa ujumla.
Jeshi hilo limesema kwamba  Mtu yeyote atakaye atakayefanikisha 
kukamatwa ikiwemo  kutoa taarifa sahihi  kwa viongozi wakuu wa jeshi la 
polisi atajipatia zawadi hiyo bila hiyana.
Namba za kupiga kama unazo taarifa sahihi ni hizi zifuatazo;
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM (CPS.H KOVA) —–0754034224
MSEMAJI WA JUESHI LA POLISI (SSP ADVERA BULIMBA)—–0713631667
MKURUGENZI WA MAKOSA YA JINAI (CP DIWANI ATHMAN)—-0715323444
Aidha wananchi wenye taarifa husika pia wanaweza kuonana uso nkwa uso
 na viongozi wakuu wa makao makuu ya polisi au kanda maalum na kuwapa 
taarifa moja kwa moja
Jeshi  hilo  limesisitiza kuwa   mwananchi ambaye ataleta taarifa 
husika na kufanikisha zoezi hilo itakuwa  siri kubwa na hatajulikana 
popote kama yeye ndiye mtoa taarifa husika.

