Mpekuzi blog
CCM inapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wake na kwa umma wa Watanzania. 
Kufunga Kampeni
CCM
 itafunga kampeni zake kwa utaratibu mpya na kwa kishindo. Kampeni za 
CCM zitafungwa kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa 
mitano. Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM kitaifa waliopo 
madarakani na wastaafu. Mikoa hiyo na viongozi wakaoongoza mikutano hiyo
 ni kama ifuatavyo:
  
1.
 Mwanza – Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John 
Pombe Magufuli, Mgombea Urais, na Ndugu Samia Hassan Suluhu, Mgombea 
Makamu wa Rais
2. Tanga – Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM
3. Mbeya – Ndugu Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
4. Mtwara – Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
5. Kigoma – Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
6. Kilimanjaro – Ndugu Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu
7. Mara – Ndugu Joseph Warioba, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu
Kati
 ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka. Mikutano hii 
itaanza saa sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya 
moja kwa moja ya vituo vya televisheni vitano na vituoa vya redio 67. 
  
Vilevile,
 watakaohudhuria katika mikutano hii wataunganishwa moja kwa moja na 
mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na 
wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia 
screens zitakazokuwa katika viwanjani vyote hivi saba.
Namna
 hii ya ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha 
nguvu ya CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku 
moja katika maeneo mbalimbali nchini. Lakini pia tutafanya historia 
katika tasnia ya utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na 
kuunganisha kwa pamoja matukio saba kwa wakati mmoja.
Kwa
 upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa 
kampeni za Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, leo, 
Ijumaa, tarehe 23 Oktoba 2015. 
  
Siku
 ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya 
Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa
 namna mahsusi.
Tathmini ya Kampeni
Kama
 Chama, tumeridhika na ubora na ukubwa wa kampeni tulizofanya licha ya 
changamoto za hapa na pale. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wamefanya kazi
 kubwa, na kwa bidii kubwa, na maarifa makubwa. 
  
Wamekuwa
 barabarani kwa siku 57 wakifanya mikutano kati ya 8 hadi 12 kwa siku. 
Imani yetu ya ushindi inatokana na kazi kubwa waliyofanya. Pia, CCM 
inawashukuru viongozi, wapenzi wa washabiki wake – wa makundi mbalimbali
 ya kijamii - kote nchini kwa kazi kwa kazi kubwa ya kampeni 
waliyoifanya.
Kutokana
 na kazi kubwa na nzuri iliyofanyika, na kutokana na mwenendo wa tafiti 
huru na tafiti zetu za ndani, CCM inategemea ushindi wa asilimia 
zisizopungua 69.
Uchaguzi wa Amani
CCM
 haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu. Sisi kama
 chama kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi wengi zaidi, na chenye 
dhamana ya uongozi wa dola, tutatimiza wajibu wetu wa kuhimiza utulivu 
kwa wapenzi, washabiki na wanachama wetu. Tunawataka na wenzetu wafanye 
hivyo.
Kauli
 za wenzetu kwamba kura zitaibiwa ni kauli za kutojiamini na kujiandaa 
kufanya vurugu. Kauli za kwamba washabiki wa UKAWA wakishapiga kura 
wabaki vituoni kulinda kura si kauli za wanaotaka uchaguzi wa amani.
Kwa
 utaratibu wetu wa uchaguzi, utaratibu wa pekee kwa Chama kulinda kura 
zake ni kwa kupitia wakala wa vyama waliopo kwenye kila kituo cha kupiga
 kura na wenye nguvu na mamlaka ya kisheria ya kushuhudia zoezi zima, 
kuanzia kupiga kura, kuhesabu kura hadi kutangaza matokeo. Kura 
zinapigwa na kuhesabiwa vituoni mbele ya wasimamizi wa uchaguzi, 
mawakala wa vyama na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi.
Mawakala
 wa vyama na wasimamizi wa uchaguzi wanaweka sahihi kwenye fomu za 
matokeo, na matokeo hayo yanatangazwa na kubandikwa kwenye kituo. Kwenye
 kituo kikuu cha Tume cha kujumlisha matokeo, mawakala wa vyama pia 
huwepo na Tume hujumlisha matokeo kutoka kwenye fomu za matokeo za vituo
 vya nchi nzima zilizosainiwa na mawakala wa vyama kwenye kila kituo.
Kwa
 viongozi wa UKAWA kuwaambia watu waingie barabarani au kuvizunguka 
vituo vya kupigia kura eti ili kulinda kura hakuna maana yoyote zaidi ya
 kutafuta namna ya kuhalalisha vujo, vurugu na uporaji na kuwazuia watu 
wengine, hasa wanawake, kupiga kura. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na 
usalama vizuie hili jambo kwasababu halina nia njema.
Mkakati
 wa UKAWA ni kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mazingira 
ya mgogoro wa kisiasa ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na 
kupendekeza kugawana madaraka. Mkakati huo hautafanikiwa. Tunaviomba 
vyombo ya ulinzi na usalama vihakikishe ulinzi na usalama wa watu wote 
na mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.
CCM haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwasababu tu ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.
  
Siku
 ya Jumamosi, CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote 
ili siku kabla ya uchaguzi, siku ya uchaguzi na mara baada ya uchaguzi, 
waweze kupiga simu au kutuma ujumbe pale watakapokuwa wanabaini au 
kushuhudia vitendo vya kuvuruga amani na kuvuruga utaratibu mzima wa 
uchaguzi.
Kupokea Matokeo
CCM
 imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia mawakala wake moja kwa
 moja vituoni na kupitia mtandao wa Chama. CCM inategemea kuwa na 
matokeo ya uchaguzi nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya uchaguzi, 
tarehe 25 Oktoba 2015.
Imetolewa na:
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni
22 Oktoba 2015.