Tundu Lissu ‘anusa’ bao la mkono Singida Mashariki 
Mgombea
 ubunge wa jimbo la Singida mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu  
Antiphas Mughwai Lissu, amesema kwamba anahofia uchaguzi mkuu  hautakuwa
 huru na wa haki akidai kwamba Jeshi la Polisi limeandaliwa kuhakikisha 
yeye hatangazwi kuwa mshindi. 
Lissu
 alisema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mkoani humo 
ambapo alibainisha kuwa amepata taarifa kupitia njia ya simu kutoka kwa 
meneja  wa mkoa wa benki moja mjini hapa na askari polisi wawili, kwamba
 jeshi la polisi limeandaa nguvu kubwa kupindua maamuzi ya wapiga kura, 
ili mgombea wa CCM atangazwe mshindi
Tundu 
 Lissu ambaye ni Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, alisema kwa nyakati 
tofauti, alipigiwa simu na askari polisi wawili akiwemo wa FFU, na kumpa
 taarifa ile ile aliyopewa na meneja wa benki.
Alisema
 askari hao walimwambia kuwa jeshi la polisi litatumia magari matatu ya 
dareya (yanayotumika kumwaga maji ya kuwasha) na kundi kubwa la askari 
na kwamba wameagizwa na viongozi wao,wahakikishe liwalo na liwe, yeye 
(Tundu) hatangazwi kushinda ubunge.
Mgombea
 huyo alisema kwa akili ya kawaida, jeshi la polisi halipaswi kutuma 
nguvu kubwa jimbo la Singida mashariki ambalo toka kampeni zianze, 
hapajatokea tukio au dalili za uvunjivu wa amani.
Katika
 hatua nyingine, Tundu Lissu ameahidi kwamba endapo atashindwa kihalali,
 atakubaliana na matokeo na hatakuwa na kinyongo chochote.Lakini endapo 
atashindwa kwa mbinu chafu, hatakubaliana na matokeo hayo machafu.
Naye 
 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP Sedoyeka, alisema 
wamemtaka Lissu kwa kuwa ni mwanasheria, athibitishe tuhuma zake hizo, 
ndipo jeshi la polisi liweze kuchukua hatua stahiki.
Katika jimbo hilo  Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemsimamisha  Bw.Jonathan Njau kupambana na Tundu Lissu katika uchaguzi huu