Aunt Ezekiel Alimwa Talaka
Kuna madai kwamba, Aunt Ezekiel alishaandikiwa talaka na ipo 
nyumbani kwa wazazi wa aliyekuwa mumewe, Sunday Demonte, Temeke Mwisho 
jijini Dar.
Kwa mujibu wa chanzo, talaka hiyo iliandikwa na mumewe huyo baada ya 
kupata taarifa kwamba, mkewe huyo ana ujauzito unaodaiwa kuwa ni wa 
Mnenguaji wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moze Iyobo.
“Hivi mnajua kwamba, Aunt alishaandikiwa talaka? Kama hamjui mjue 
sasa. Ipo Temeke kwa wakwe zake. Jamaa si yupo Uarabuni mahabusu, 
alisikia mkewe ana mimba ya Iyobo.  Nadhani wanashindwa kumpa hiyo 
talaka kwa sababu walishakata mawasiliano naye tangu kitambo,” kilisema 
chanzo.
Aunt mwenyewe alipotafutwa juzi  na kuulizwa kuhusu madai hayo,  alisema: 
“Sijui lolote kuhusiana na hilo, aliyesema kuwa nimeandikiwa talaka ipo ukweni kwangu ndiye angesema kila kitu yeye kwa vile anajua, mimi sijui.”
Credit:Gpl 

 
No comments:
Post a Comment